Katika Darsa hili, amewausia Wanafunzi kuomba Dua njema kwa Mwenyezi Mungu ili awapatie na kuwaruzuku daima Vitu vizuri vitakavyokuwa ni sababu ya kuzifurahisha Nyoyo na Nafsi zao kwa kuvitizama.
Sheikh Mtulia, akitoa ufafanuzi Muhimu katika Darsa lake kwa Wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania.
Ametoa mfano hai kuhusu hilo kama vile mtu kuomba Mwenyezi Mungu akuruzuku kupitia Mke wako Mtoto Mwema atakayekuwa furaha ya macho kwa kumtizama, kama alivyokuwa Sayyidat Fatima (s.a) kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).
Your Comment